Mgombea
urais kwa niaba ya chama cha Republican, Trump ambaye anaongoza hivi
sasa katika kinyang'anyiro hicho, amesema siasa zake za mambo ya nje,
zitaweka maslahi ya Marekani mbele.
Katika
mahojiano na gazeti la New York Times amesema nia yake sio kwamba
anataka kuitenga Marekani ila anasema anapanga kusitisha kupunjwa kwa
Marekani na washirika wake.
Amesema
anataka Marekani iache kuendelea kununua mafuta yake kutoka Saudia hadi
pale waSaudi watakapokubali kupeleka majeshi yao kupigana na wanamgambo
wa IS.
Aidha
Trump ameongeza kusema kuwa endapo ataibuka mshindi wa uchaguzi wa
urais wa Marekani, atayaondoa majeshi ya Marekani kutoka Japan na Korea
Kusini kama mataifa hayo hayatailipa zaidi Marekani kwa wanajeshi hao
kuendelea weko nchini humo.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )