WAZIRI wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe leo amemsimamisha
kazi Mkurugenzi Msimamizi wa Wanyamapori, Charles Mulokozi baada ya
kutoa vibali vya kusafirisha Tumbili kwenda Albania.
Sakata hilo limetokea baada ya Jeshi la Polisi kuwakamata raia wawili wa
Uholanzi katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)
wakiwa na tumbili 61 hai wakijaribu kuwasafirisha kwenda nchini Albania.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )