Habari
kutoka visiwani Zanzibar zinaeleza kwamba, nyumba kadhaa ikiwemo ya
Hamdani Omar Makame ambaye ni Kamishna wa Polisi Viswani Zanzibar
zimelipuliwa kwa mabomu.
Habari
hizo zinaeleza kwamba, Jeshi la Polisi linaendesha kamata kamata ya
watu waliohusika kwenye tukio hilo ambapo mpaka sasa watu 31
wametiwa mbaroni.
Tukio
hilo limezidisha hali ya wasiwasi visiwani humo ambapo ni siku 5 tu
zimesalia kabla ya uchaguzi wa marudio kufanyika
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )