Mkazi
wa Gongo la Mboto, Omary Hamis (25) amehukumiwa kifungo cha maisha jela
baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mtoto wa miaka tisa ambaye ni
mlemavu wa kusikia na kuongea.
Hakimu
Mkazi, Flora Haule wa Mahakama ya Wilaya ya Ilala, alisema mahakama
imeridhishwa na ushahidi wa mashahidi tisa ukiwamo wa daktari na fomu
namba tatu ya polisi (PF3), iliyotolewa mahakamani hapo kama kielelezo
dhidi ya mshtakiwa huyo.
“Mahakama
imekukuta na hatia hivyo inakuhukumu kifungo cha maisha jela, baada ya
kupatikana na kosa la kumlawiti mvulana wa miaka tisa ambaye ni mlemavu
wa kusikia na kuzungumza, ili iwe fundisho kwa jamii,” alisema hakimu Haule.
Katika
ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, ilidaiwa kuwa mtoto huyo siku ya
tukio alifika kwenye banda la kuonyeshea video ambalo linamilikiwa na
Hamisi saa za jioni, kwa ajili ya kuangalia video, lakini Hamis
alimfukuza kutokana na kutokuwa na pesa ya kiingilio.
Baada
ya kumfukuza mtoto huyo aliondoka, lakini baadaye alirudi bila ya Hamis
kuwa na taarifa akakaa ndani ya banda na kisha kupitiwa na usingizi
uliosababisha abaki kwenye banda hilo peke yake hadi usiku.
Hamis alitumia mwanya huo kumlawiti mtoto huyo kwenye jumba bovu lililopo jirani na ofisi yake hiyo.
Mashahidi
waliieleza mahakama kuwa walisikia sauti ya mtu ambayo ilikuwa
haisikiki vizuri akiomba msaada, ndipo waliposogea na kumkuta Hamis
akitekeleza kitendi hicho huku akijua kuwa ni kosa kisheria.
Mashahidi
walidai hata walipomkaribia, Hamis aliendelea kutekeleza kitendo hicho
hadi walipolazimika kumpiga mateke. Hamis alikiri kuwa siku hiyo watoto
walifika kwenye banda lake hilo.
Wakili
wa Serikali, Ester Kyara aliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa
mtuhumiwa ili iwe fundisho kwa wote wanaotumia mabanda ya kuonyesha
video kufanya ukatili kwa watoto.
Katika
utetezi wake, Hamisi alisema ana familia inayomtegemea hivyo apunguziwe
adhabu, maombi ambayo yalitupiliwa mbali na mahakama hiyo na kuhukumiwa
kifungo cha maisha jela.
Hamisi anadaiwa kutenda kosa hilo Agost 26, 2014 eneo la Gongo la Mboto.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )