Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amefunguka na kusema Chama Cha Mapinduzi CCM ni kile kile cha siku zote, Zitto Kabwe amesema hayo baada ya kusoma vitabu vya Bajeti ya mwaka huu na kusema kuwa bajeti hiyo ni ya kulipa deni la Taifa.
Kwa Mujibu wa Zitto Kabwe amedai kuwa Serikali inatarajia kukusanya shilingi trilion 17 kwa mwaka na kusema zaidi ya tirioni 8 zitakwenda kulipa deni la Taifa ambalo ni zaidi ya asilimia 50 ya bajeti na kusema ukichanganya na mishahara ya watumishi ambayo huwa ni nusu ya bajeti ni dhahiri kwamba makusanyo ya Serikali yataishia kulipa madeni na wafanyakazi.
"Nimemaliza kusoma vitabu vya Bajeti ya mwaka huu. Kimsingi ni Bajeti ya kulipa Deni la Taifa.
Wakati Serikali inatarajia kukusanya shilingi trilion 17 mwaka huu, shiling trilioni 8 ikiwa ni asilimia 50 italipia Deni la Taifa. Ukiweka na mishahara ya watumishi ambayo huwa ni nusu ya bajeti, ina maana makusanyo yote ya Serikali yatalipia madeni na mishahara.
Ndiyo maana Serikali inaenda kukopa zaidi ya shilingi trilion 7 mwaka huu na kutegemea misaada ya wafadhili kwa shilingi trilion 5. CCM ni ile ile, ile ile....." aliandika Zitto Kabwe
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )