Featured
Loading...

Simba SC yamsimamisha Abdi Banda Mwezi Mmoja Kwa Utovu wa Nidhamu...

 
Klabu ya Simba SC ya jijini Dar es Salaam imemfungia mwezi mmoja beki wake, anayeweza kucheza nafasi za kiungo pia, Abdi Banda baada ya kumgomea kocha Mganda, Jackson Mayanja kuingia katika mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Coastal Union.

Simba imemfungia Banda tangu Aprili Mosi mwaka huu na mchezaji huyo natarajia kurejea kikosini mwishoni mwa mwezi huu.

Banda alimgomea kocha Mganda, Jackson Mayanja kuingia dakika ya tano katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union, kuchukua nafasi ya Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, akidai ni mapema mno kumtoa beki mwenzake kwa sababu ya makosa machache aliyofanya.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top