Kesi
ya Lyatonga Mrema kupinga ushindi wa Ubunge wa James Mbatia jimbo la
Vunjo ilikua Mahakamani tena April 4 2016 ambapo jipya lililotangazwa ni
kwamba Mahakama kuu kanda ya Moshi imeridhia makubaliano yaliyofikiwa
kati ya Mbunge wa Vunjo James Mbatia na Agustino Mrema kwa shauri hilo
kuisha na kwamba Mbatia ndiye Mbunge halali wa Vunjo na Mrema atatakiwa
kulipa sehemu ya gharama za mawakili wa Mbatia shilingi Milioni 40.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )