Featured
Loading...

KR Mullah Ajibu Tuhuma Na Sir Nature Kuhusu TID na Matumizi ya Madawa ya Kulevya


Mwanamuziki KR Mullah amefunguka baada ya msanii mwenzake wa kundi la Wanaume Halisi Juma Nature, kusema kitendo cha KR kujiunga na Radar Entertainment, huenda kitamuharibu asipokuwa makini.

KR Mullah, amemtaka Juma Nature amuache kwa sasa afanye kazi, kwani kwa sasa anataka kubadilisha ladha ya muziki wake na huenda hajapendezwa na yeye kuingia Radar Entertainment na kuachana na Wanaume Halisi.
“Nilikuwepo ndani ya kundi la wanaume halisi, sasa labda anavyoona mimi nipo huku anaona kazi zake tena zitakuwa zinalegalega, pengine labda hakupendezewa mimi kwenda kufanya kazi na yule mtu na kwamba yeye alitegemea mi nifanye kazi naye,” alisema

Sambamba na hilo KR, amemuongelea TID ambaye Juma Nature alimtahadharisha kuwa makini nao wasije wakamuingiza kwenye matumizi ya madawa ya kulevya kuwa  hajawahi kumuona kutumia vitu hivyo.

“Kusema kweli zamani nilikuwa nasikia sikia hizi taarifa, lakini yeye mwenyewe alitangaza kuacha muda mrefu, lakini kwa sasa tangu nimeanza kukaa naye sijawahi kumuona akiitumia au akifanya hayo mambo, muda mwingi tunapiga stori za kikazi zaidi” alisema KR Mullah

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top