Mashabiki wengi walionekana kumkosoa kwa uamuzi wake wa kubandika kipini puani huku wengine wakionekana kuwa waelewa wa kile alichokifanya.
Swali ambalo linazunguka kwenye vichwa vya mashabiki na wapenzi wengi wa muziki je, ni kweli Chibu katoga pua yake?
Meneja wake Sallam, aliamua kutegua kitendawili hicho na kaamua kuandika kwenye mtandao wa kijamii, akisema msanii wake huyo aliamua tu kuwashtua watu si kweli kwamba ametoboa pua.
“Usiamini kila unachoona kwenye picha au unachoambiwa, mlikuwa mmelala sana amewaamsha kidogo,” aliandika Sallam
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )