Featured
Loading...

Rais Magufuli Apiga Simu Clouds TV Na Kutaja Mshahara Wake Anaolipwa....Asema Akitoka Likizo Ataonyesha Nyaraka za Malipo




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. John Pombe Magufuli amempigia simu mtangazaji wa kipindi cha ‪Clouds360‬ cha ‪‎CloudsTv‬, Hudson Kamoga baada ya kusikia watu wanazungumzia kuhusu mshahara wa Rais.

Rais amesema mshahara alioukuta na ambao analipwa  ni milioni 9 na laki 5 (9,500,000)   na  wala  sio milioni 30  kama  wanavyodai wapinzani. Amelazimika kuyasema hayo wakati wa uchambuzi wa magazeti kupitia Clouds360.

Ameahidi akirudi kutoka likizo yupo tayari kuonyesha nyaraka za malipo ya mshahara wake.

Gazeti  la  Nipashe toleo  la leo lilikuwa na habari  iliyowanukuu Tundu Lissu  na  Zitto Kabwe wakitaka Rais Magufuli ataje Mshahara wake na aweke wazi kama anakatwa kodi ili kuondoa sintofahamu iliyopo .
 
Hivi karibuni, Dk. Magufuli ameahidi kupunguza mishahara ya baadhi ya vigogo inayozidi shilingi milioni 15 ili mtumishi anayepata mshahara mkubwa zaidi usizidi kiasi hicho.

SHARE

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top