Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli,
tangu iingie madarakani moja ya ajenda ambayo imekuwa ikisisitizwa ni
kuweka mazingira safi ambapo, Rais Magufuli mwenyewe aliongoza kampeni
hiyo na kampeni hiyo imeendelezwa na watendaji wengine wa serikali
akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
April 30
2016 viongozi mbalimbali, wasanii na wananchi walifanya usafi maeneo
mbalimbali ya jiji la Dar es salaam na baadae kufanya matembezi kutoka
maeneo ya Ilala, Temeke na Kinondoni na kukutana Leaders Club ambako
imezinduliwa rasmi kampeni ya siku 90 ya Dar es salaam kuwa safi.
Mkuu wa Mkoa Dar es salaam Paul Makonda ameizindua kampeni hiyo na amezungumza haya……..
>>>’tuliacha
nafasi ya 2015 na kurudi nyuma kwamba kila mmoja atafanya usafi kwa
sababu anajua ni wajibu wake lakini kwa kuwa tumeshindwa kutumia fursa
hiyo sasa acha tufanye usafi kwa kushurutishwa na mamlaka tuliyopewa na
Rais’
>>>’kamanda
Sirro anajua kwamba amri yangu ni utekelezaji sitaki kuona biashara ya
daladala inapitapita hapa mjini siku ya jumamosi nataka kuona usafi
unafanyika na baada ya pale saa 3 tutafanya biashara zetu‘;-Paul Makonda
Aidha Paul Makonda amemuagiza
Katibu Tawala wa Mkoa kuunda kamati ili kuchunguza makampuni ya usafi
kama yapo yanayomilikiwa na watumishi wa umma kwa sababu inakiuka sheria
ya utumishi wa umma…….
>>>’tunao
watumishi wa umma wameanzisha makampuni ya kusafisha miji yetu lakini
kwa kwa mujibu wa maadili ya utumishi wa umma kuna kipengele cha
mgongano wa maslahi kwa hiyo RAS ninakuagiza ukatangaze Kamati
itakayochunguza makampuni yote‘
>>>’zaidi
nataka hiyo kamati iende kuangalie makampuni haya yanayoshinda tenda
mengi hayana vifaa kama yalivyoeleza kwenye makaratasi yao:-Paul Makonda
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )