April 29 2016 Mbunge wa Muleba Kusini na aliyewahi kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka amefanya Exclussive Interview na AYO TV na kuzungumzia hatua ya Rais John Pombe Magufuli kuanzisha Mahakama ya Mafisadi Nchini.
Profesa Tibaijuka anasema………>>>’Kwanza ukishaanzisha Mahakama unatafuta haki na ukweli, Watanzania wanahukumu kwa wepesiwepesi, sio kila mtuhumiwa ni mkosaji‘
>>>’Kwahiyo
hili ni jambo zuri, sio kila mtuhumiwa ana kosa, kuna mitandao ya
mafisadi inahakikisha kwamba haikamatwi na kuwapeleka wenzao mbele ndio
inasema kafara, hivyo tunataka majipu yawe majipu haswa sio kukamua
nyama tukamue majipu yenyewe‘
Yeye pia alikuwa na tuhuma za rushwa, anasemaje katika hili? …>>>’Ukweli
ndio umeniweka hapa Bungeni, Wananchi wangu walielewa kuwa sio jambo
nililohusika nalo, ikumbukwe mimi nilikuwa Waziri wa Ardhi na fedha
zilitoka Benki kuu, sasa Waziri wa Ardhi na Benki kuu wapi na wapi?’
‘Ndio maana suala hili la kuwa na mahakama ni zuri sana, kwasababu kule Mahakamani ndio kuna nafasi ya kuujua ukweli‘
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )