WAUMINI wa Kanisa Katoliki na Madhehebu
mengine ya Kikristu kote duniani, juzi Alhamisi ilikuwa ni siku ya
kuabudu Sakramenti ya Ekarist Takatifu ikiwa ni ishara ya kuanza kwa
safari ya mateso, kifo na ufufuko wa Yesu Kristu, Ibada ambayo kwa
kawaida hufanyika matukio mbalimbali likiwemo la waumini kuoshwa miguu.
Katika tukio la waumini kuosha miguu,
kiongozi wa ibada (padri, askofu, kardinali au papa) huchagua viongozi
wa jumuiya, usharika, kigango, parokia au jimbo katika kanisam hilo kama
wawakilishi wa waumini wengine na kuwaosha miguu yao kama ishara ya
upendo kwao na kuwafuta makosa yao kama alivyofanya Yesu Kristu
alipowaosha miguu mitume wake 12 kabla ya kula nao karamu ya mwisho ya
Pasaka.
Juzi ilikuwa tofauti kwa Kiongozi Mkuu
wa kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis baada ya kuamua kutembelea
kituo kimoja cha wakimbizi kilichopo Castelnuovo di Porto, nje ya Mji wa
Roma, kuwaosha miguu na kuibusi bila kujali itikadi ya dini zao.
Wakimbizi hao walikuwa ni wa madhehebu ya Kiislam, Orthodox, hindu na
wakatoliki. Papa aliosha miguu wanaume, wanawake na watoto.
Wakati akiiwasili kwenye kambi hiyo,
Papa Francis alikaribishwa kwa mabango yaliyokuwa yameandkiwa kwa lugha
tofauti yakimaanisha neno “Karibu”. Aliendesha ibada ya misa takatifu
hapo ambayo ilihudhuriwa na maelfu ambao kati yao, watu 892 walikuwa ni
wakimbizi waliohitaji hifadhi.
Wakimbizi hao walionesha kufurahishwa na
kitendo cha Papa Francis kuwatembelea na kufanya nao ibada ya kuwaosha
miguu huku wengine wakionekana kuchukua picha za na video za ukumbusho
wa tukio hilo kuu duniani wakitumia simu zao za mkononi (smartphone).
Papa Francis hakusita kuelezea kuguswa
kwake na namna ambavyo wakimbizi wanavyoteseka, safari yake ya kwenda
Mexico anavyotumia muda wake mwingi kuwaombea wakimbizio hao ili wawe na
amani na nchi zao ziondokane na machafuko.
Hii imekuwa tofauti kidogo na
ilivyozoeleka kwamba sheria za kanisa kuwataka wachungaji kuwaosha miguu
wanaume pekee, lakini Januari mwaka huu Papa Francis alibadili sheria
hiyo ili kutoa nafasi kwa wanawake na mabinti kushiriki zoezi hilo
duniani kote. Papa alianza kwa kuwaosha miguu na kuwabusu wanaume 12
akiashiria kama yesu alivyowafanyia mitume wake, baadaye papa aliwaosha.
Taarifa ya kutoka Makao Makuu ya Papa,
Vatican Italia, imeeleza kuwa, Papa alichagua wanawake wanne na wanaume
nane ambapo miongoni mwa wanawake hao ni raia wa Italia mmoja, Eritrea
watatu. Wanaume walikuwa wakatoliki wanne raia wa Nigeria, Waislam
watatu wa Mali, Syria na Pakistan na Mhindu mmoja wa India jambo ambalo
halijawahai kutokea kwa kanisa katoliki.
Sheria hiyo mpya inaelekeza kuwa kila
mtu ni ametoka kwa mungu, hivyo anahaki ya kutafakari mateso, kifo cha
Yesu na kusherehekea ufufuko wake.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )