Msanii Hakeem 5 ambaye alitambulika
katika muziki baada ya kufanya Collabo na msani Ali Kiba kwenye wimbo wa
‘Nakshi Mrembo’ amefunguka na kusema kuwa msanii Ali Kiba si mtu mzuri
na wala hana muda nae kwa sasa.
Akipiga stori kwenye kipindi cha Planet
Bongo cha East Africa Radio ambapo leo alipewa heshima ya Bongo fleva,
Hakeem 5 anadai kuwa msanii huyo kwa sasa amekuwa akijisikia sana kitu
ambacho yeye kimemkera na kudai kuona kwamba msanii huyo ana roho mbaya,
roho ya kukunja.
” Unajua kuna wasanii wana roho mbaya
sana wanadhani kwamba ridhiki wao ndiyo wanatoa kumbe Mungu ndiye mtoaji
wa ridhiki, kiukweli kabisa Ali Kiba kwa sasa sitaki hata kumsikia
sababu huyu jamaa nampigia simu simu zangu hata hapokei, ujumbe wangu
hajibu na kuna siku nilikutana nae studio na kumwambia naomba tufanye
kazi pamoja lakini yeye aliniambia unajua, Hakeem 5 kazi tutafanya ila
subiri kwanza na mambo kama hayo ndiyo maana saizi sitaka hata kumsikia”
alisema Hakeem 5.
Katika hatua nyingine msanii huyo
amezidi kusikistiza kuwa anataka kufanya kazi na msanii huyo na kusema
kuwa yeye hataki pesa za Ali Kiba ila anachotaka kwa sasa ni kufanya nae
kazi tu, kwani yeye Hakeem 5 anasema ameshamalizana na Ali Kiba kwenye
wimbo wa Nakshi Mrembo ila Ali Kiba yeye bado hajamalizana na msanii
huyo.
Unajua mimi nimefanya mambo makubwa na
Ali Kiba na wala hakunilipa na mimi sitaki pesa zake nilimwambia sitaki
pesa yako mimi nataka tufanye kazi, yeye anasema kila jambo linawakati
wake, mimi nilishamalizana na yeye ila yeye hajamalizana na mimi” alidai
Hakeem 5.
eatv.tv
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )