Baada ya rapa Chidi Benz kuomba msaada
ili asaidiwe kuirudisha afya yake ambayo imethorofika kutokana na
matumizi ya Madawa ya kulevyana na baadae kusaidiwa na Babu Tale kwa
kupelekwa rehab. Wadau mbalimbali pamoja na wasanii wenzake walimpongeza
Babutale lakini Dudu Baya amedai hakupenda rapa huyo asaidiwe.
Akizungumza na Bongo5 Jumamosi hii, Dudu
amedai rapa huyo hakuwa tayari kusaidiwa ndio maana baada ya kusaidiwa
anataka kujipangia baadhi ya mambo.
“Watu mfano wa Chidi Benz hawatakiwi
kusaidiwa, niwakuachwa wafe na wazikwe. Kwanza ni waongo, ukikutana nao
utasikia naumwa au nimefiwa, utampa msaada, mwisho wa siku anaenda
kujidunga. Misaada kama hii inatufanya majina yetu kuwekwa kataka orodha
ya wauaji (killers),” alisema Dudu.
Aliongeza, “Babutale na wenzake
walipomfisha Chidi Benz rehab kwanza alianza kuweka masharti yake
kituoni, mara hawezi kushauriwa na mtu ambaye hajawahi kutumia sumu hiyo
(unga). Hapo ndipo nilipogundua amebebwa kinguvu bila yeye kuwa tayari
kupona. Ni sawa na mgonjwa apelekwe hospitali then aanze kutoa masharti
yake, eti hiki kitanda sikitaki. Wewe dokta huwezi kunitibu kwa sababu
hujawahi kuumwa ugonjwa ninaoumwa, mgonjwa kama huyo si nachotaka ni
kifo?. Hata wakati yesu amekuja kutukomboa na dhambi, aliponya wagonjwa
waliokuwa tayari kupona, hata leo umpeleke ndugu yako kanisani au
msikitini akaombewe aache ulevi au umalaya, kama hana dhamira ndani ya
moyo wake ya kuacha, hakiwezi tokea chochote,”
Pia Dudu amesema wasanii wengi wanasikia kila siku kuhusu madhara ya Madawa ya kulevya lakini wanapuuzia.
“Chidi Benz si mtoto mdogo, ameshuhudia
wasanii na watu wa kawaida wengi tukiwapoteza kwa sababu ya Madawa ya
kulevya lakini wanapuumzia, wanarudia kubwia tena. iweje leo yeye
ajiingize kataka ulimwengu huo? hakika kifo anakitaka mwenyewe na si
kurubuniwa. Uzuri wa Tanzania hatuna umasikini wa ardhi, watu kama hawa
hawana faida kwa taifa, niwakuacha wafe na wazikwe. Na kama inawezekana
Mh Rais Magufuli angetoa amri mateja wakifa wazikwe na jiji. Kwa sababu
sioni ndugu yeyote wa Chidi yuko bize na rapper huyo. Kwanini nyingi
mumpaparikie au ndio mnauchukungu kuliko ndugu zake?. Asiyefunzwa na
mamaye hufunzwa na ulimwengu,” alisema Dudu.
Bongo5
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )