Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda Jumapili iliyopita alitoa simulizi ya enzi hizo akielezea jinsi
baba yake mzazi alivyomnasa vibao kwa sababu ya kung’ang’ania shule.
Alisimulia mkasa huo wakati akizungumza
na watu walioalikwa katika semina maalum ya kampeni iliyoitwa Mimi ni
Nani, Shtuka Mapema iliyofanyika katika Ukumbi wa Josam House jijini
Dar, ambako alisema baba yake hakusoma hata darasa moja wakati mama yake
aliishia darasa la saba, lakini wote wawili hawakujua umuhimu wa elimu.
“Siku moja nilijifungia chumbani
nikaanza kulia, mara baba akaja na kunikuta natoka machozi na makamasi,
akaniuliza kwa nini nalia, nikamwambia nataka kwenda shule. Nililambwa
makofi kwelikweli, sitasahau siku hiyo. Hii ni kwa sababu baba hakujua
umuhimu wa elimu,” alisema Makonda.
Akaongeza: “Baba alitaka niwe mkulima wa
nyanya kwa sababu siku hizo zao hilo lilikuwa na soko nchini Kenya
lakini mama kwa upande wake aliunga mkono ndoto zangu za kusaka elimu.”
Akifafanua zaidi alisema, kutokana na king’ang’anizi chake alifanikiwa kusoma hadi Chuo Kikuu na kuwa rais wa vyuo vikuu vyote nchini na kuleta mabadiliko makubwa kielimu kwani alitetea mambo mengi ya wasomi na yakafanikiwa.
“Hivi sasa baba nikimkatia tiketi ya ndege kuja Dar anasema nikatie ndege ya jioni ndiyo nzuri…” alisema Makonda na kusababisha ukumbi mzima kuangua kicheko. Aliwataka wasomi na watu wengine kutimiza ndoto zao badala ya kutegemea kuambiwa na watu au kusoma vitabu walivyoandika wenzao.

“Unajua kuna mtu aliyegundua umeme
utokanao na maji lakini yupo mtu mwingine akakuna kichwa na akafikiri
akaona kwa nini asitengeneze umeme kwa kutumia jua, akafanikiwa,
mwingine akaona kwa nini asitengeneze umeme kwa kutumia makaa ya mawe,
akajaribu na kufanikiwa… huu ndiyo ubunifu unaotakiwa,” alisema.
Katika semina hiyo wanasemina
walihimizwa kufanyia kazi ndoto zao ambapo Kampuni ya Global kupitia kwa
mwakilishi wao, Elvan Stambuli iliwaomba washiriki kucheza Bahati
Nasibu ya Shinda Nyumba kwa kukata kuponi zinazopatikana katika magazeti
ya Risasi, Uwazi, Amani, Wikienda, Ijumaa na Championi ili kujiongezea
fursa ya kujishindia nyumba ya kisasa.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )