Nimeileta
hii mada huku kwa makusudi kwakuwa inahusika na mapishi lakini vile
vile na afya zetu kwakuwa mapishi na afya haviachani
Sehemu
kubwa ya mboga za Darisalama zinatoka mabonde ya Mto Msimbazi, Mandela
road bonde lililoko kituo cha garage, Jangwani, Kigogo sambusa na maeneo
ya Tandale na kwingineko
maji
yanayopita kwenye mabonde haya ni machafu, yenye kemikali toka
viwandani, yenye vinyesi toka vyooni nk ndio hayo hayo yanayonyweshea
mbogamboga hizi tangu kuchipua hadi kukomaa.
Kwa
vyovyote vile, maji haya yakipimwa ni wazi yatakutwa na kiwango kikubwa
cha sumu mbalimbali zinazosababisha magonjwa kansa na ngozi.
Uchafu
tunaoutupa kwenye mito ipitayo kwenye haya mabonde kama betri za simu
na magari material za friji mbovu, computer mbovu nk nk vyote hivi
vimebeba kemikali zenye sumu kali.
Tusipochukua tahadhari tutaishia kuongeza vyumba pale Ocean road kwenye ile hospital ya kansa
By Mshana JR/Jamii Forums
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )