Ukimya wa aliyekuwa mgombea wa Urais wa UKAWA,Edward Lowassa umezua
mjadala kwenye mkutano wa Kamati Kuu ya CCM.Kikao cha Kamati Kuu
kimefanyika jana hapa Dodoma.
Mjadala ulianza pale Mwenyekiti Kikwete alipochagiza maelezo yake ya
chama kuendelea kufanya maandalizi ya chaguzi zijazo na kutobweteka.
Mwenyekiti alisema kuwa Lowassa bado ana uungwaji mkono na nguvu ya
kisiasa na hutumia ukimya kujijenga zaidi.
Mwenyekiti alionya kuwa Lowassa hakufika mwisho na chama chapaswa
kuutazama ukimya wake wa kuchangia na kutoa hoja juu ya Serikali ya Rais
Magufuli kwa jicho la tatu. Wajumbe wote wa KK walikubaliana na
Mwenyekiti Kikwete.
Wakati huohuo,Rais Magufuli ameaswa kuwa 'mpole kiasi' atakapoukwaa
uenyekiti wa taifa wa CCM mnamo mwezi Juni mwaka huu. Imesemwa kuwa
wanachama wa chama cha siasa hutendewa mambo kwa upole ili wabaki
chamani na kukijenga chama. KK imeunga mkono hatua za Rais na Serikali
yake kutumbua majipu!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )