Na. Immaculate Makilika – MAELEZO
Serikali
 ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa 
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, imefanya jitihada kadhaa ikiwa ni 
sambamba na kutekeleza  sera mbalimbali ambazo zimeiwezesha nchi ya 
Tanzania kupata mafaniko makubwa ndani na nje ya nchi katika kipindi  
cha miaka mitatu
Akizungumza 
 jana jijini Dar es salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na 
Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi, ametaja mambo 10 muhimu  
yaliyofanywa na  Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais wa 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika kipindi 
cha miaka mitatu na ambayo yameitangaza nchi ya Tanzania kimataifa.
Dkt.
 Abbasi alitaja mambo hayo kuwa ni uchumi unaoendelea kukua kwa kasi 
nzuri, ambapo  katika mwaka 2017/18 uchumi wa Tanzania ulikua kwa 
wastani wa asilimia 7.1 na kuongoza katika nchi zote za Afrika 
Mashariki, huku  ukiingia katika rekodi ya kuwa miongoni mwa nchi ambazo
 uchumi wake unakua kwa kasi zaidi duniani kama ambavyo  ripoti 
mbalimbali za kimataifa zimeeleza.
“Uchumi
 wetu ni wa tisa kwa ukuaji wa kasi duniani na katika Afrika, Kusini mwa
 Sahara ni wanne, hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya World Economic Forum 
ya mwezi  Machi, 2018 na kwa nchi za Afrika Mashariki  uchumi wa 
Tanzania unaongoza kwa ukuaji” alisema Dkt. Abbasi
Kuongezeka
 kwa mapato ya Serikali katika kipindi cha miaka mitatu, Rais Magufuli 
amethubutu kuziba mianya ya upotevu wa mapato na kuongeza kasi ya 
kukusanya kodi na hivyo kuongeza mapato ya kodi ya Serikali kutoka 
wastani wa shilingi  bilioni 850 kwa mwezi hadi kufikia wastani wa  
shilingi trilioni 1.3 kwa mwezi.
Kufufuliwa
 kwa mashirika ya umma, Dkt. Abbasi alisema kuwa kutokana na 
ufuatiliaji, ubunifu, uwekezaji wa Serikali ya Rais Magufuli, mashirika 
mengi  mfano  Shirika la Mawasiliano Tanzania(TTCL), Shirika la Reli 
Tanzania (TRC) na Mamkala ya Maji Safi (DAWASA) na Bandari  sasa 
yameanza kuamka kuwa na ufanisi, kuongeza mapato na mengine kutengeneza 
faida.
“Baadaa
 ya Serikali kuchagiza mageuzi ya kiutendaji sasa  kwa mwaka TTCL  
inakusanya shilingi bilioni 212 kutoka shilingi bilioni 102, Bandari 
imekusanya kutoka shilingi bilioni 703 hadi kufikia shilingi bilioni 838
 kwa mwaka, TRC kutoka shilingi bilioni 23 hadi 36 kwa mwaka  na DAWASA 
shilingi bilioni 32.4 hadi shilingi bilioni 122.4 kwa mwaka “ alisema 
Dkt. Abbasi
Aidha,
 Dkt. Abbasi alisema kuwa katika kipindi hiki cha miaka mitatu Serikali 
ya Rais Magufuli imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika sekta ya  viwanda 
ambapo jumla ya  viwanda 3,306 viliandikishwa, na vingine vinaendelea 
kujengwa na baadhi vimekamilika. Halikadhalika viwanda hivyo vimeanza 
kutengeneza  bidhaa mbalimbali ambapo kati ya hivyo viwanda 251 ni 
vikubwa na vya kati ni 173.
Ambapo
 mchango wa ekta ya viwanda katika pato la Taifa umeongezeka kutoka 
asilimia 5.2 mwaka 2015 hadi 5.5 mwaka 2017. Kasi ya ukuaji wa Sekta ya 
Viwanda ilikua kutoka asilimia 6.5 mwaka 2015 hadi asilimia 7.1 mwaka 
2017/18.
Akiendelea
 kufafanua mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano Dkt. Abbasi alisema 
kuwa Rais Magufuli amepambana na rushwa na ufisadi kwa pamoja na mambo 
mengine, sambamba na  kutimiza ahadi yake ya kuunda Makosa ya Uhujumu 
Uchumi maarufu kama Mahakama ya Mafisadi
“Mpaka
 sasa kesi mpya 41 zimefunguliwa, na  kuna maombi ya dhamana 346 
yamewasilishwa katika Mahakama hii kati ya mwaka  2017 na 2018” alisema 
Msemaji huyo wa Serikali.
Katika
 sekta ya usafirishaji nako, Serikali ya Rais Magufuli imefanya mageuzi 
kadhaa, yaliyopelekea sekta hiyo kupata mafaniko  ya kuwa  na  ndege nne
 mpya zinazoendelea kuleta mageuzi katika usafiri wa anga nchini, abiria
 wanaotumia ndege za ATCL wameongezeka kutoka takribani abiria 4,000 kwa
 mwezi hadi abiria 30,000 kwa mwezi.
Aliongeza
 kuwa  ndege mbili   aina ya Air Bus zenye uwezo wa kubeba abiria watu 
132 zitawasili nchini Disemba mwaka huu, na ndege aina ya  Boeing 
dreamliner ya pili inatarajiwa kuwasili nchini Oktoba mwaka mwakani.
Aidha,
 mradi wa umeme wa Stigler’s gorge utakapokamiika unatarajiwa kuzalisha 
 megawati 2,100, sambamba na mradi wa ujenzi wa reli kwa kiwango cha 
standarg gauge kutoka Dar es salaam hadi Morogoro na baade Dodoma, 
ambapo umefikia 33% ya ujenzi.
Mafaniko
 mengine ya Serikali hii yanaonekana katika katika sekta ya afya,  
ikiwemo kujenga vituo vya Afya vya Kata 210 na kukarabati vingine vingi 
kufikisha idadi ya vituo vinavyotoa huduma hadi mwaka huu kuwa 7,746 
kutoka vituo 7,014 mwaka 2014/15 sawa na ongezeko la asilimia 10.4.
 Dkt.
 Abbasi  alifafanua kuwa vituo hivi pia vina wodi za kina mama na vifaa 
vya kisasa. Aidha, ajira zaidi ya 6,000 za kada ya afya zimetolewa. 
Katika miaka mitatu Zahanati zimeongezeka kutoka 6,143 mwaka 2015 hadi 
6,646 mwaka huu ikiwa ni sawa na  ongezeko la zahanati 503  ambapo 
baadhi zilijengwa na zingine kukarabatiwa sawa na ongezeko la asilimia 
8.1.
Vilevile,
 Serikali ya Awamu ya Tano imefanya mageuzi ya kiutendaji ikiwemo 
kuongeza Bajeti ya Dawa na Vifaa Tiba kutoka shilingi bilioni 31 mwaka 
2015 hadi kufikia shilingi bilioni 270  kwa mwaka huu wa fedha.
Ongezeko
 hilo limewezesha upatikanaji wa dawa muhimu katika vituo vya kutolea 
huduma za afya nchini kufikia asilimia 89.6 kutoka asilimia 36 mwaka 
2015/16. Aidha upatikanaji wa dawa muhimu umepanda kutoka wastani wa 
asilimia 35 tu hadi asilimia 93.
Sekta
 ya madini nayo, Dkt. Abbasi alisema kuwa “Serikali iliweka lengo la 
kukusanya shilingi bilioni 1.5 kwa mwaka kutoka kwa wachimbaji wadogo wa
 Tanzanite pale Mirerani. Hata hivyo kabla hata ya nusu ya mwaka huu wa 
bajeti kufika, tayari mapato eneo la Tanzanite yamefikia shilingi 
milioni 788.5 sawa na asilimia 52 ya lengo la mwaka 2018/19, hii 
inashadidisha kuwa uamuzi wa Mhe. Rais kujenga ukuta ulikuwa makini” 
alisema Dkt. Abbasi
Katika
 miaka hii mitatu licha ya matukio ya hapa na pale, Tanzania imeendelea,
 kusimama kama moja ya visiwa vya amani duniani na  Taifa limeendelee 
kushikamana kawa kuishi kwa amani na upendo.
Aidha,
 Dkt, Abbasi  alisema kuwa Rais Magufuli anasimamia misingi na 
Watanzania leo wako huru  kuamua mambo yao kama Taifa, huku akisisitiza 
 kuwa safari ya kujitegemea imeanza  na mataifa mbalimbali duniani  
yanafahamu   azma ya Rais Magufuli kwa Taifa lake.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
 

 
 
 
 
 
 
 
