Na Imma Msumba Arumeru,
Mkuu
 wa Wilaya ya Arumeru kwa kushirikiana na Jeshi la polisi Wilaya ya 
Arumeru limewakamata watuhumiwa wa Tatu ambao wameshiriki kumtoa mimba 
mwanafunzi wa kidato cha nne kwa kutumia dawa za miti shamba suala 
ambalo linachochea mimba kwa wanafunzi na kuzorotesha elimu yao.
Dc
 Muro amesema kuwa wamebaini tukio hilo baada ya kuweka mtego na 
kuwabaini watuhumiwa hao pamoja na mtia mimba ambao wamefikishwa polisi 
kwa ajili ya kufikishwa mahakamani
Akielezea
 jinsi alivyopewa ujauzito na kisha ujauzito kutolewa aikaeli Pallangyo 
amesema ni kweli alipata ujauzito Kwa kurubuniwa na kijana wanaeishi nae
 Jirani nyumbani ambae alikuwa akimrubuni Kwa kumpatia fedha
Kwa
 upande wao watuhumiwa wa sakata hilo kijana aliempa mimba Binti,pamoja 
na mama Mzazi wa Aikaeli na mwanamke ambae ni ndugu wa Kijana aliempa 
mimba ambae anatajwa kuhusika na kumtoa ujauzito Binti wametoa sababu 
mbalimbali ambazo hata hivyo zimeonekana kukinzana zenyewe Kwa zenyewe 
Kutokana na mama wa Binti kukiri Kuwafahamu watuhumiwa wenzake na 
kuelezea tukio la Mchezo mzima ulivyokuwa
Akidhibitisha
 taarifa Za Binti huyo kuwa mjamzito na kutoa ujauzito, Mganga mkuu wa 
halmashauri ya Meru Daktari Cosmas kilasara amesema vipimo vya awali 
vilionyesha Binti kuwa mjamzito na vipimo walivyofanya tena vimeonyesha 
Binti sio mjamzito tena ambapo amesema hata hivyo Binti huyo ameendelea 
kupata dalili zote Za kuwa na ujauzito ikiwemo ya maziwa kutoka.
Kutokana
 na tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru amevigiza vyombo vya Usalama 
kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote ambao wamehusika katika tukio 
hilo , ambapo pia amelitaka jeshi la Polisi kuhakikisha wanawakamata na 
wanawafikisha mahakamani watu wote waliohusika katika kuwapa ujauzito 
wanafunzi 57 Kwa kipindi Cha miaka miwili iliyopita.
Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
 

 
 
 
 
 
 
 
