Mei 4 2016 Bunge limeendelea Dodoma ikiwa ni mkutano wa tatu, kikao cha kumi na mbili ambapo katika kipindi cha maswali na majibu Mbunge Mgeni Jadi Kadika viti maalum aliulizwa swali kwa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Swali lake lilikuwa ni…>>>’Ugonjwa
wa Myoma ni moja kati ya matatizo makubwa yanayoathiri akina mama
kuzuia uzazi na kusababisha kansa ya kizazi pamoja na kupoteza maisha.’
‘Je, ni kwa kiasi gani Serikali imefanikiwa katika kuwasaidia akina mama wanaoteseka na matatizo haya?’
Majibu yakatoewa na Naibu Waziri Hamisi Kigwangalla…>>>’Myoma au kwa jina la kitaalamu unajulikana kama ‘Uterine Fibroid’ ni uvimbe unaoota kwenye misuli ya tumbo la uzazi wa mwanamke.’
‘Chanzo
halisi cha Myoma hakijulikani ila kila Myoma huanza kwa ukuaji hovyo wa
seli moja, ambayo hutoa protini kwa wingi. Tafiti pia zimeonyesha Myoma
hutokana na mabadiliko ya vinasaba kwenye seli za Myoma ambazo
hubadilisha ukuaji wa seli hizo.’
‘Myoma
ni uvimbe ambao siyo Saratani, na hauna tabia ya kubadilika kuwa
saratani. Myoma ikiwa kubwa huweza kuonyesha dalili kama kuvimba tumbo,
kuvuja damu kwa wingi na maumivu makali ya tumbo chini ya kitovu‘
‘Serikali
huwahamasisha wakina mama wote kupima afya zao kabla ya kushika
ujauzito, wakati wa ujauzito hata baadaya kujifungua. Japokuwa siku
hizi kuna dawa ambazo daktari anaweza kumpatia mama kabla ya uvimbe kuwa
mkubwa‘
‘Aidha,
kama uvimbe umekaa sehemu ambayo haufai kutolewa wenyewe na mamaa
amekwishamaliza kuzaa basi hushauriwa kutoa mfuko wa kizazi (uterus)‘
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )