Moja ya vitu nilivyovipenda Brazil ni walivyojipanga kwenye usafirishaji…. wingi wa watu haujafanya vituo vyao vya Mabasi viwe vichafu au visivutie, sheria za Mabasi yanayotumika ndio kama yanayoonekana kwenye picha na barabara zao za umbali mrefu zimetenganishwa kwa umbali kiasi kwamba hakuna uwezekano wa magari kugongana uso kwa uso.
Kwenye haya mabasi mfano ukisafiri kutoka mji mmoja kwenda mwingine hakuna kondakta ndani, Dereva ndio anafanya kazi ya kuhakiki majina ya kila anaeingia kwenye basi baada ya kununua Ticket baada ya hapo ni safari tena Mabasi mengi yakiwa na huduma ya WiFi ndani, yani Internet unaipata bure safarini na mabasi yote ni sharti yawe na choo ndani.
Vituo vya Mabasi vimezibwa kwa juu hivyo hata mvua ikinyesha sio tatizo Abiria kushuka au kupanda kwenye basi.
Mabasi
haya ni ya gorofa, ukiwa na uwezo zaidi unalipia kukaa kwenye sehemu
yenye hadhi zaidi ndani ya basi ambako mnakaa wachache na unanafasi ya
kulala na kujisevia vinywaji.
Abiria wanakaa juu na chini na niliambiwa kwa chini ndio unalipia pesa nyingi zaidi na mnakaa wachache.
Hapa ni ndani ya kituo cha Mabasi kwenye mji wa Sao Paulo
Sehemu za kukata ticket ndani ya kituo
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )