Usiku wa Mei 2 2016 ndio ulikuwa usiku wa kihistoria kwa klabu ya Leicester City toka ianzishwe miaka 132 iliyopita, huenda unafahamu kama Leicester wametwaa
Ubingwa lakini hujui kama Ubingwa huo ndio Ubingwa wao wa kwanza katika
historia ya klabu hiyo. Mtu wangu wa nguvu naomba nikuletee mambo 10.
1- Kabla ya kutwaa Ubingwa msimu Leicester City ilikuwa haijawahi kutwaa Ubingwa wa Uingereza.
2- Mafanikio yake makubwa EPL ni kushika nafasi ya pili mara moja msimu wa 1928/1929
3- Leicester imekuwa ikipanda na kushuka Ligi Kuu Uingereza katika vipindi 13.
4- Msimu wa 2012/2013 Leicester City walitinga nusu fainali ya Ligi daraja la kwanza na walicheza na Watford.
5- Msimu wa 2013/2014 walifanikiwa kupanda daraja na kushiriki EPL msimu wa 2014/2015.
6-
Baada ya kupanda EPL na kushiriki msimu wa 2014/2015 walimaliza wakiwa
nafasi ya 14 kabla ya hapo robo ya msimu walikuwa nafasi ya mwisho
katika hatari ya kushuka daraja.
7- Msimu wa 2014/2015
Leicester walikaa nafasi ya mwisho katika msimamo wa Ligi kwa siku 140
na kuweka rekodi ya katika historia ya EPL.
8-
Kocha wao Claudio Ranieri amewahi kufundisha vilabu 14 vikiwemo vilabu
vya Chelsea, Atletico Madrid na Inter Milan hakuwahi kushinda taji la
Ligi Kuu.
9- Claudio Ranieri wakati
anaingia kuifundisha Leicester City hakuwahi kupewa imani na wachambuzi
wa soka Uingereza kutokana na CV yake ya vilabu alivyofundisha.
10- Kauli ya kwanza ya Claudio Ranieri baada ya kupewa kibarua hicho
“Nilisema ni ngumu sana kupata mafanikio Ligi Kuu ndani ya msimu
wa pili Ligi Kuu, malengo yangu ni kuhakikisha namaliza msimu nikiwa na
point 40 tu”
CHANZO: AZAM TV
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )