May 3 2016 ilikuwa ni zamu ya Wizara ya  Kilimo, Mifugo na Uvuvi kuwasilisha bajeti yake ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2015/2016, Waziri husika akiwa ni  Mwigulu  Nchemba ambaye ndio alipata nafasi ya kuwasilisha bajeti hiyo.
Wabunge waliopewa nafasi ya kuchangia baada ya bajeti kuwasilishwa ni pamoja na Kangi Lugola Mbunge wa  Mwibara aliyesema ‘Mheshimiwa
 Mwenyekiti kama kanuni zinaruhusu kuna majipu pale nje uyaruhusu 
yaingie ndani na uyaulize kila Mbunge ni mahali gani yamuote mwilini 
mwake, hakuna atakayekubali yamuote sehemu za siri‘
‘Rais
 ametumbua watumishi hewa ila Wizara ya Kilimo ina watumishi hewa na 
wakulima hewa hao inabidi uwatumbue Mheshimiwa Mwigulu Nchemba‘
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )