Featured
Loading...

Rich Mavoko ashoot video akiwa na Diamond SA, kutambulishwa WCB ‘soon’


Diamond Platnumz alimpeleka Rich Mavoko kwenda kushoot video ya wimbo wake mpya na wa kwanza akiwa chini ya Wasafi Records, imebainika.


Mavoko anadaiwa kuwa ameshasaini kuwa chini ya record label hiyo inayokua kwa kasi kitambo tu lakini uongozi unasubiri hadi video yake itakapokamilika ndipo atambulishwe rasmi.


Diamond na Mavoko walienda Afrika Kusini May 16 na ofcourse hawakusema chochote zaidi ya muimbaji huyo wa ‘Make Me Sing’ kuweka picha hiyo juu akiwa kwenye ndege na kuandika: On Another Move…. Eeh Mwenyez Mungu nibarikie na Hii…. pray #WcbWasafi.”

Mavoko anakuwa msanii wa tatu kuwa chini ya WCB baada ya Harmonize na Raymond.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top