Featured
Loading...

#TrendingWorldwide: Jina jipya katika list ya Rappers matajiri duniani, mtoto kapata mkwanja kutoka facebook, kisa?


Kama hukupata nafasi ya kuisikiliza Amplifaya ya Clouds FM May 4 2016 kutokana na kukosa time mtu wangu wa nguvu naomba nikuletee stori mbili zilizoingia kwenye headlines za Trending World Wide kwa siku ya leo May 4 2016.
1.Rapper Drake ametangazwa na Forbes kuingia katika list ya rappers matajiri duniani akiwa katika nafasi ya tano ya Rappers wenye utajiri mkubwa zaidi duniani. Forbes ilimtangaza Drake kuwa na utajiri wa dolla milioni 60 ambazo ni zaidi ya bilioni 130 za kitanzania.drrake
Utajiri wa Drake umechangiwa na ziara zake za muziki, nyimbo anazotoa ambazo zinamuingizia mkwanja  kupitia mauzo ya mitandao, dili za Sprite na Nike pamoja na Albamu yake mpya ya ‘VIEWS’ ambayo iliuza zaidi ya kopi 630,000 siku alipotoa na kumuingizia  bilioni1.9 za kibongo.
2.Uongozi wa Facebook ambao pia unamiliki appilication ya Instagram, umemzawadia mtoto wa miaka 10 kutoka Finland  dola elfu 10 ambazo ni zaidi ya milioni 20 za kibongo, baada ya kugundua udhaifu katika application ya Instagram ambapo angeweza kufuta comments za watu wengine hata kama sio katika ukurasa wake.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top