Featured
Loading...

Kama umesikia stori za Sanchez kujiunga na Juventus


Najua watu wangu wa nguvu wanaopenda soka la ulaya, huu ni wakati ambao wanafuatilia kwa karibu mipango na uboreshwaji wa timu wanazozishabikia, headlines za usajili wa wachezaji soka ndio zinatawala kwa sasa, najua utakuwa ulisikia stori za Alex Sanchez wa Arsenal kuhusishwa kujiunga na Juventus ya Italia.
Mkurugenzi wa klabu ya Juventus ya Italia Giuseppe Marotta ameamua kuweka wazi ukweli kuhusiana na stori hizo za Juventus kumuhitaji Sanchez, Marotta amesema ni kweli Juventus wanamuhitaji Sanchez lakini wanajua haiwezi kuwa rahisi kwa Arsenal kumuachia nyota huyo ajiunge nao.
Alexis-Sanchez
Sanchez aliyejiunga na Arsenal mwaka 2014 kwa ada ya uhamisho unaotajwa kufikia pound milioni 35 akitokea klabu ya FC Barcelona ya Hispania, amebakiza mkataba wa miaka miwili wa kuendelea kuitumikia Arsenal, lakini klabu ya Arsenal pia inaripotiwa kutaka kumuongezea mkataba ili asije kuondoka Emirates

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top