Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala nchini, limekifutia usajili wake wa kutoa huduma za kitabu, Kituo cha Tiba Asilia cha ForePlan Kliniki kilichopo Ilala Bungoni jijini Dar es salaam, kinachomilikiwa na Dkt. Juma Mwaka maarufu kama Dkt. Mwaka, kwa madai kuwa kimekiuka taratibu za kitabu za tiba mbadala.
Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dkt. Edmund Kayombo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, kwenye Ukumbi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Akizungumza jijini Dar es salaam leo katika Mkutano na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Dk. Edmund Kayombo amesema kuwa kufutiwa kibali cha Dk. Mwaka kunatokana na sababu nyingi ambazo amekuwa akikiuka licha ya kupewa maonyo na barua juu ya utoaji huduma zake.
Amesema sababu nyingine ni kuwa katika matangazo yake amesema anatoa tiba za kisasa wakati hiyo elimu hana ya kufanya huo.
Wengine waliofutiwa usajili ni Fadhaget Sanitarium kinachoendeshwa na Tabibu Fadhili Kabujanja pamoja na Mandai Herbal Clinic kinachoendeshwa na Tabibu Abdallah Mandai
Hata hivyo limetoa adhabu mbalimbali kwa kituo cha Aman Herbal Clinic kinachoendeshwa na Tabibu Esbon Baroshigwa, na Tabibu Castory Ndulu wa Kituo cha Ndulu Herbal Clinic wamepewa barua ya onyo.
Aidha wengine wamesimashwa kwa miezi sita ambao ni Tabibu John Lupimo wa Lupimo Suntarium Herbal Clinic pamoja na Tabibu Simon Rusigwa wa Sigwa Herbal Clinic.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )