Hilo Zari alilielezea kwa mafumbo kwenye Snaochat na kudai kuwa hajali kama nchini au ukoo usipomkubali, ilimradi tu wanapendana na mpenzi wake.
Tetesi nyingine ni kuwa staa huyo wa ‘Utanipenda’ si mwaminifu kwenye uhusiano wao na kwamba huenda akawa na ukaribu usio wa kawaida na Hamisa Mobetto.
Yote hayo yanaonesha kuwa si kitu kwenye couple hii na wameamua kuonesha kuwa wapo strong kupitia Instagram. Wamepost picha na video kadhaa wakiwa na mtoto wao Tiffah kuashiria kuwa mambo ni shwari.
“Sending love from the other side from me and mines. Have a blessed week,” ameandika Zari kwenye post moja wapo.
Naye Diamond akiwa na familia yake hiyo ameandika, “Aint nothing better than spending time with the people that you love from the bottom of your heart……hata ukiwa kijuso, ukiwa nao kasura kanakuwaga kama kanapata Uhendisamu kwa mbaaaali kwa furaha
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )