Featured
Loading...

Mchina Amuua Mfanyakazi wake kwa kumpiga, kisa kaomba aongezewe Mshaahara


Kijana mmoja aliejukikana kwa jina moja ( Elisha) mkazi wa  Kabindi Mkoani Geita ammefariki Dunia baada ya kupigwa na mchina kwa jina Mr. Swii kwa madai ya kusadikika kwamba alilalamika ili wapandishiwe ongezeko la mshahara, kwa maelezo kamili waliopigwa wengine wawili wako hospital kwa matibabu zaidi.

Marehem alipo pigwa akaenda Hostitali na baada ya hapo aliambiwa arudi kazini huku hali yake ikiwa mbaya na ndipo alipodondoka na kuzimia ndipo wakafanya jitihada ya kumpeleka hospital ya Mkoa na kufariki Dunia, tukio hili limetokea katika Mgodi wa Nyamahuna uliopo Katoro Mkoa wa Geita. Mgodi huu unachimba Dhahabu na Shaba.

Mashuhuda wanasema kuwa Mr Swii pamoja na walinzi wa Mgodi huo ndio waliohusika katika kuwapiga Wafanyakazi hao nakupelekea mfanya kazi mmoja kufariki Dunia kwa Kipigo hicho.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top