Featured
Loading...

Mkono Apongeza TRA Kumfungia Ofisi zake


Baada ya hivi karibuni, Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA kuzifungia Ofisi za Mbunge wa jimbo la Butiama Mkoani Mara Nimrold Mkono kwa kudaiwa malimbikizo ya kodi, Mbunge huyo ameibuka na kuisifu mamlaka hiyo kwamba ilikuwa sahihi kufanya hivyo na kupongeza juhudi zinazofanywa na Serikali awamu ya Tano katika ukusanyaji wa mapato.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Bw. Mkono amesema kuwa ulipaji wa kodi si kwa ajili ya wafanyabishara pekee, bali ni wajibu wa kila Mtanzania wakiwemo viongozi wa Serikali na kuongeza kuwa kitendo cha TRA kufunga Ofisi yake inayotumika kwa shughuli za uwakili ilikuwa sahihi kwani walitimiza wajibu wao kwa ajili ya kuboresha uchumi wa taifa.

Kampuni ya Nimrold Mkono inayojishughulisha na masuala ya Uwakili ilifungwa kwa kudaiwa Kodi ya Shilingi Bilioni Moja lakini hata hivyo Ofisi tayari imefunguliwa na kuendelea na shughuli zake.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top