Featured
Loading...

Mourinho kataja TOP 3 ya wachezaji wake bora wa muda wote na kumpotezea Ronaldo


Kocha mpya wa Man United Jose Mourinho ameingia tena kwenye headlies baada ya kutoa kauli ambayo imesambaa katika mitandao ya jamii, Mourinho katika mahojiano na Daily Express ametaja majina ya wachezaji wake watatu wa muda wote na kumuacha Ronaldo.
Mourinho amewataja Messi, Pele na Diego Maradona kama ndio wachezaji bora wa muda wote na kumpotezea mreno mwenzake Cristiano Ronaldo ambaye wengi walikuwa wanatarajia kuwa atakuwemo katika list ya Mourinho ukilinganisha uwezo wake na utaifa wao“Kwangu mimi binafsi TOP 3 ya wachezaji bora wa muda wote katika historia ni Messi, Pele na Maradona”
071916-SOC-real-madrid-cristiano-ronaldo-jose-mourinho.vadapt.664.high.86
Ronaldo aliwahi kufundishwa na Mourinho kwa misimu mitatu ndani ya klabu ya Real Madrid lakini mwaka 2012 alifanikiwa kushinda tuzo ya Ballon d’Or chini ya Mourinho tena, kauli ya Mourinho inatafsirika kama kuwa na tofauti na Ronaldo lakini wengi hawakutarajia kuona Ronaldo akikosekana katika list hiyo.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top