Akiongea Jumanne hii wakati wa kuapishwa kwa wakurugenzi wapya ikulu jijini Dar es Salaam, alisema alikuwa akicheka tu alivyokuwa akisoma comments za wananchi kuhusu uteuzi wake huo.
Anadai comments zilizomshangaza ni kuwa mmoja wa wakurugenzi hao ni msomi wa cheti cha usimamizi wa hoteli wakati anajua aliyemteua ni msomi wa shahada ya uzamili ya usimamizi wa biashara, MBA.
Aliwatania waandishi wa habari wampige picha mkurugenzi huyo aitwaye Luhende aliyekuwepo kwenye hafla hiyo na yule wanayemdhania ni mfanyakazi wa hoteli Sinza.
Hivi karibuni Rais Magufuli aliwateua wakurugenzi 120.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )