July 17 2016 headline kutoka Ikulu Dar es salaam ni pamoja na hii Rais
John Pombe Magufuli kumteua Profesa Longinus Rutasitara kuwa makamu
mwenyekiti wa bodi ya mamlaka ya usafiri wa anga (TCAA), Rutasitara
anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk. Nyamajeje Weggoro ambaye muda
wake umemalizika.
Pia Rais Magufuli amempandisha cheo kamishna msaidizi wa Polisi (ACP)
Kedmon Mnubi kuwa kamishna msaidizi mwandamizi wa polisi (SACP)
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )