Featured
Loading...

Sakata la Lugumi: Mbona Tunababaishwa?


Mwanzoni,ilitolewa taarifa kuwa PAC iliunda Kamati Ndogo kuchunguza zaidi sakata la mkataba wa kampuni ya Lugumi. Kamati hiyo ndogo ilipewa wajibu wa kwenda kujionea ufungwaji wa mashine za utambuzi wa alama za vidole katika vituo vya polisi.

Kamati ndogo ilitarajiwa kuandika na kuwasilisha ripoti ya uchunguzi wao kwa PAC. PAC ilipaswa kupokea ripoti ya kamati yake ndogo,kuijadili,kuamua na kuiwasilisha Bungeni. Haikufanyika hivyo. Makamu Mwenyekiti wa PAC Hilary Aeshi aliahidi kuwa Ripoti ya Lugumi ingewasilishwa katika mkutano ujao wa Bunge.

Jana,Naibu Spika Dr. Tulia Ackson ni kama ameifunga hoja ya Lugumi. Akijivika mamlaka ya Bunge zima,Dr. Tulia alitoa maagizo kwa Serikali kuhusu mashine za Lugumi. Vipi kuhusu kashfa ya kimkataba? Kwanini tunababaishwa hivi kuhusu sakata la Lugumi?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Singida)

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top