Kama utakuwa unakumbuka hivi karibuni msanii wa Bongo Fleva, Baraka Da
Prince kutoka kwenye label ya Rockstar 4000 aliingia kwenye headlines
baada ya mpenzi wake Najma kuonekana kuwa kama mkalimani wake kwenye
interview ya MTV Base.
Baraka Da Prince na kuyaongea ya moyoni:
Baraka Da Prince na kuyaongea ya moyoni:
Unajua watanzania asilimia kubwa wanakuwa wanakurupuka sana mimi sijaona kwanza kitu cha ajabu cha mimi kutumia lugha ya Kiswahili, mimi nimeenda MTV Base nimeulizwa Je unataka kutumia lugha gani ili uwe huru nikawajibu ninaweza nikatumia lugha ya Kiingereza lakini sitokuwa huru’–
‘Sasa wabongo walifurahi wengine wakasema nimeshindwa kuongea kingereza kwangu mimi nimeitangaza lugha yangu ya kiswahili halafu Najma hakuwa mkalimani wangu mimi bali alikuwa anawambia yule mtangazaji kile ninachokizungumza mimi’- Baraka Da Prince
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )