Featured
Loading...

Chanjo mpya ya HIV kujaribiwa Afrika Kusini


Chanjo dhidi ya virusi vya ukimwi itaanza kutumika nchini Afrika Kusini mwaka huu baada ya kukidhi vigezo vinavyohitajika na kuthibitisha kwamba ina uwezo wa kusaidia kupambana na
janga hilo barani Afrika.

Watu 2.1 million waliambukizwa virusi vya ukimwi mwaka 2015 barani Afrika, theluthi mbili ya maambukizi hayo yalitokea kusini mwa jangwa la sahara.

Watu 252,000 waliandikishwa ama kupokea chanjo ijulikanayo kama ALVAC-HIV/gp120, au placebo kwa kulinganisha kiasi gani cha kinga kinatengenezwa mwilini kwa muhusika.

Matokeo yatawasiliswa leo tarehe 21/07 katika mkutano wa kimataifa wa AIDS mjini Durban, Afrika kusini.
Chanjo kama hii ilifanywa nchini Thailand mwaka 2009 na ilionyesha uwezo mkubwa  wa kumkinga mtu dhidi ya virusi vya ukimwi kwa asilimia 31%.

Chanjo hii imeboreshwa zaidi kwa ajili ya matumizi ya nchi zenye hatari ya kuwa na maambukizi zaidi zilizo kusini mwa jangwa la sahara, ambapo kuna aina tofauti za virusi hivyo.

Watu wapatao 5400 katika miji minne tofauti nchini Afrika kusini watapata chanjo hii Novemba  na kuwa nayo kwa mda wa miaka mitatu

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top