“Mimi nimefanya collabo na Chid, kipindi hicho nilimwambia, hakunitoza hata sh. kumi wala hakunizungusha hata kidogo, ndio maana linapokuja suala la Chidi nakuwa wa kwanza, wakati mimi namfuata Chidi, Chidi hasa nikajua atanikatalia kwanza mimi mbana pua, lakini hakunizungusha na wala hakuniomba hata mia”, alisema Diamond Platnumz.
Tujikumbushe hivi karibuni msanii Chid Benzi alipata matatizo ya matumizi ya madawa ya kulevya, na Diamond alichukua jukumu la kumpeleka hospitali na kumbadilisha damu, kabla hajapelekwa rehab kupata tiba ya urahibu.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )