Mwimbaji
wa nyimbo za Injili nchini Emmanuel Mbasha amesema anaomba radhi kwa
mashabiki wake wote ambao walikuwa wanafuatilia habari zake kuhusiana na
kutengana na mke wake Flora Mbasha na yeye kukataa kuzungumzia habari
hizo kwa muda wote.
Akizungumza
na EATV kipindi cha FNL, Mbasha amesema hapendi kuzungumzia mambo yake
na Flora Mbasha kwa sababu tayari Mungu amemshindia kesi ya ubakaji
iliyomkabili na baadaye akaweza kushinda hivyo hapendi kumzungumzia tena
mambo hayo.
”Kesi
nimeshinda na amenishindia Mungu hivyo sipendi kuzungumzia mambo hayo
tena, na hata wanasheria wangu wamenishauri nisizungumzie tena mambo
hayo, ila kikubwa ninachowaomba mashabiki wafuatilie sasa ni nyimbo
yangu mpya ya ‘Haribu Mipango ya Shetani” ambayo imetengenezwa na
mtayarishaji wa nyimbo Pablo.
Aidha
Msanii huyo amesema hajarudiana na Flora Mbasha na yupo Single kwa sasa
na anachokifanya kikubwa kwa sasa ni kumtumikia Mungu.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )