Leo(Jana)
nimewatembelea ndugu zangu wa Kilolo - Iringa kuwashukuru na kuwaeleza
kuwa tulishinda na ndio maana hawa mabwana wakubwa wanapata tabu sana Na
Sisi.
Miezi
michache iliyopita nilitangaza kuanza ziara ya kushukuru wananchi kwa
kura Million 6 wakazuia mikutano ya hadhara na kama haitoshi wakazuia
mikutano ya ndani pia ninayotaka kuhudhuria ,imefikia mahala wanatisha
hadi wafanyabiashara wanaotukodishia kumbi za mikutano.
CHADEMA
chama chetu ni kikubwa sana , kinawatesa , tumewachapa kweli kweli
uchaguzi Mkuu 2015, tumewashinda katika majiji na miji mikuu kiasi
wanapata Tabu , wageni toka Nje wakija pale Airport Rais huwa anaulizwa
kuhusu mameya wetu na anapata kigugumizi kutambulisha kuwa hawa ni
wapinzani.
Ni jambo la kufurahia na sababu ya sisi kutokata tamaa.
Ni ishara kwamba tunaweza.
Pili
Uchaguzi Mkuu ujayo 2020 tutashinda tukiwa wamoja , tuwe wamoja na
wanajua sisi ni wamoja . Na nawasihi tuendelee kuwa wamoja hivi hivi,
tusiruhusu vitisho vitutenganishe.. Hakuna nguvu kubwa kama ya Umma.
Uongozi ni dhamana na njia pekee njema ya kuongoza ni meza ya makubaliano na sio vitisho kwa wananchi kama ilivyo sasa.
KUHUSU UKUTA .
Jambo
hili la UKUTA ni kubwa mno si jambo dogo hata kidogo .Jana balozi wa
Marekani aliwatumia ujumbe raia wake wajiandae kuondoka tarehe 1
September kwa hofu walionayo. Hata Mimi nina hofu kama tusipotekeleza
hili nchi itakuwa wapi hapo baadae. Haiwezekani mtu mmoja ajiamulie tuu
kila jambo na kuvunja katiba .
Wasuluhishi
wanasema tuzungumze , tunakubali kuzungumza ,lakini tuzungumze nini
ikiwa mtu anavunja Katiba na hawamuonyi hawamshauri hii si sawa kabisa.
Mtu
mmoja anajiamulia kuvunja katiba anazuia mikutano anazuia mikutano ya
ndani na wasuluhishi hawamuonyi ,nasema kabla ya kuja kwetu wakamueleze
yeye kwanza matendo yake .
POLISI
niwaeleze duniani kote maandamano ni haki ya msingi kabisa , police
wakiua raia au wanachama wetu tuwaarifu dhahiri tutagoambana nao mmoja
mmoja, hatutahangaika na jeshi tutahangaika Na Polisi aliefanya mauaji,
alie fyatua risasi ajue dhahiri tutamshitaki ICC .
Ni
bora tufilisike ,tutaabike lakini tutawalinda watanzania Na
waandamanaji wetu wote nchi nzima Kata zote kama tulivyo kubaliana.
Ni aibu vyombo vya dola vinatumia nguvu kubwa kutisha watu wasio hata na fimbo.
Tabia
za baadhi ya viongozi ni mbovu sana , wanavunja Katiba Na kukanyaga
demokrasia , hili hatuwezi kuliruhusu litokee Tanzania hata kidogo. Zipo
jitihada za usuluhishi hatuna shaka nazo lakini wajue jambo
tunalolipigania liko wazi ni Katiba wamwambie aruhusu mikutano na haki
za kidemokrasia .
Tujitokeze
kwa wingi sana September 1, tuandamane bila kuharibu Mali ya mtu kama
tulivyofanya wakati Wa kuchukua Fomu pale buguruni ,Tume hadi Kinondoni
bila hofu .
Tuna
chama Imara sana CHADEMA kinacho tetea Uhuru ,haki ya mwananchi ,
maendeleo na ustawi wa nchi . Tunawapenda sana, ninawapenda Na
Ahsanteni.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )