Hotuba fupi ya Edward Lowassa kuhusu Operation UKUTA na Ujenzi wa Chama Leo katika majimbo ya Mbeya Vijijini ,Vwawa na Tunduma.
UKUTA si fujo , UKUTA si machafuko na
hatuna haja ya kufanya fujo , tunapiga kelele dhidi ya uvunjwaji wa haki
ya kidemokrasia na katiba ya nchi unaofanywa na utawala huu wa awamu ya
tano
CHADEMA ni nani wakapambane na polisi
,polisi ambao ni watoto wetu ,ndugu zetu na hata wake na waume zetu ila
tuwahakikishie hatutorudi nyuma pale katiba na haki ya kidemokrasia
ikichezewa au kuwa chini ya mtu fulani . Najua polisi watapiga watu
,wataumiza watu na hata kuua ila niwahakikishie wao na walio na mamlaka
wataishia katika mahakama ya Kimataifa
Siasi ni mazungumzo ,lazima tuzungumze
milango yetu iko wazi kufanya mazungumzo ila kwa kuwa hawahitaji na sisi
hatutorudi nyuma September Mosi ,tumejiandaa vya kutosha na sasa tuko
ngazi ya kaya na nyinyi wajumbe mkakamilishe kazi katika kaya zenu ili
tarehe mosi sauti ya kutosha ipazwe kwa maandamano na mikutano kama
tulivyokubaliana katika kata zetu na majimbo nchi nzima . Haiwezekani
hata kidogo mtu mmoja azuie kila kitu ,nchi hii ni mali yetu sote .
Kamati kuu ilipo amua katika suala la
UKUTA haikukurupuka , kamati kuu yetu inaundwa na mchanganyiko wa wasomi
wa kada mbalimbali ,wazee wenye busara na vijana machachari kamwe
hawawezi kukukurupuka na UKUTA ni haki ya watanzania wote.
Pili naomba niwape siri ya ushindi 2020
ndugu viongozi na wanachama wenzangu , tutashinda uchaguzi Mkuu 2020
kama tutafanya yafuatayo na kuyasimamia Moja . Umoja ndani ya Chama na
wanachama ,tuheshimiane ,tusameheane na tuimarishe chama chetu ,chama
ndani ya Chama , chama nje ya chama na chama ndani ya Umma .
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )