Featured
Loading...

MCHANGANUO WA AJIRA MPYA AIR TANZANIA.

Rais John Pombe Magufuli alitangaza kuwa mapema mwezi Septemba Serikali itanunua ndege mbili kubwa aina ya Bombardier Q400 kutoka nchini Canada ili kuweza kulipa uhai shirika la ndege la Tanzania (ATCL).


Kufuatia tamko hilo tayari marubani wameshapelekwa nchini Canada kwa ajili ya mafunzo ya kurusha ndege hizo zitakazowasili nchini mwezi Septemba. Kufuatia ujio huo wa ndege mbili, ATCL inatarajia kuajiri wafanyakazi 28 watakaohudumu katika ndege hizo mbili.

Mchanganuo wa wafanyakazi hao ni kama ifuatavyo;-


  1. Shirika la Ndege (ATCL) litaajiri marubani wanne, ambao ni sawa na marubani wawili kwa kila ndege moja kwa ajili ya kurusha ndege hizo.
  2. Shirika la Ndege (ATCL) litaajiri wahandisi sita ambao ni sawa na wahandisi watatu kwa kila ndege moja. Hawa watashungulika na matengenezo ya ndege pindi inapokuwa na tatizo.
  3. Shirika la Ndege (ATCL) litaajiri wahudumu 18 ambao ni sawa na wahudumu tisa kwa kila ndege. Hawa watakuwa wakitoa huduma kwa abiria pamoja na maelekezo mbalimbali kuhusu ndege wakati wa safari.
  4. Aidha, kwa upande mwingine, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa alisema kuwa serikali imejipanga kununua rada sita mpya kwa ajili ya ndege za kiraia ili kuongeza usalama zaidi wakati wa safari za anga nchini.

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top