Featured
Loading...

Mwambaji Malaika na Aliyekuwa Mpenzi Wake Eddy Hapatoshi...Wanyanganyana Magari


MREMBO anayesumbua na Wimbo wa Rarua Rarua, Diana Exavery ‘Malaika’ na mpenzi wake aitwaye Eddy wapo kwenye bifu zito baada ya mrembo huyo kudaiwa kutaka apewe gari na mpenzi wake huyo baada ya kumwagana.

Chanzo kinaeleza kuwa, baada ya kumwagana miezi kadhaa iliyopita, Malaika alienda kumfungulia mashtaka Eddy aliyeishi naye kwa zaidi ya miaka mitatu akidai anamdhulumu gari lake.

“Yaani hapatoshi, Eddy kakataa kumpa gari, Malaika anahangaika na hana ushahidi wa kumiliki gari alilokwenda kushtaki polisi, Eddy kamaindi kuona anamletea polisi wakati si mhalifu,” kilisema chanzo.

Mrembo huyo alipotafutwa hakutaka kuzungumzia ishu hiyo lakini Eddy alipopatikana alisema Malaika atakuwa kaishiwa ndiyo maana anamfungulia kesi za ajabu lakini kamwe hatamuweza.

Source:GPL

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top