Featured
Loading...

Naj na Mr Blue wadaiwa kuwasiliana, Naj aeleza kwanini alisave namba ya Mr Blue kwa jina la ‘Zai’


Msanii wa muziki Naj amekanusha tetesi za kugombana na mpenzi wake Barakah Da Prince baada ya kudaiwa kupigiwa simu usiku wa manane na aliyekuwa mpenzi wake wa zamani Mr Blue.


Inadaiwa wakati Barakah ameshika simu ya mpenzi wake Naj, alipiga mtu ambaye namba yake ‘iliseviwa’ Zai na baada ya Barakah kupokea alikuta sio mwanamke bali ni mwanaume ambaye alidaiwa kuwa ni Mr Blue.

Akiongea katika kipindi cha U-Heard cha Clouds FM cha Jumatano hii, Naj amekiri kusave kimakosa namba ya Mr Blue kwa jina la Zai.

“Kuna watu wanaongea vibaya lakini hawajui, kwanza mimi siwasiliani na Mr Blue, unajua mimi mtu nikishakuwa naye hatuwezi kuwa marafiki, mnakuwa marafiki mnaongea nini sasa,” alisema Naj.

“Na mimi zamani sana hata kabla sijaanza mahusiano na Barakah, nikapata missed call kwenye hiyo namba, sasa mimi nikaisave ‘Zai’ kwa haraka haraka ili niingie whatsapp ili nijue ni nani, kwa sababu mimi mara nyingi nikipataga missed call sitakagi kumpigia mtu ambaye simjui, kwa hiyo baada ya kufanya hivyo ndo nikamjua ni nani. Kwa hiyo ilikuwa kitambo sana halafu mimi mwenyewe nilikuwa sijafuta wala nini na sio kwamba ni namba ambayo naitumia wala nini,” alifafanua zaidi.

Pia Naj ameeleza jinsi mpenzi wake Barakah alivyoigundua namba ya Mr Blue kwenye simu yake.

“Nilimpa Barakah simu yangu akawa anaitumia hata sijui kati yao nani alimpigia mwenzake kwa sababu namba ilikuwa kwenye majina. Kama ningekuwa na mambo mengi nisingejiamini kumpatia simu mpenzi wangu, kwa hiyo hata sijui nani alimpigia mwenzake kati yao, lakini namba ilitokea kama Zai,” alisema Naj.

Hata hivyo hivi karibuni katika kipindi cha U-Heard, rapper Mr Blue ambaye alifunga ndoa mapema mwaka huu na mwanadada aitwae Warda, alikana kuwasiliana na Naj.

Source:Bongo

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )
© Copyright MZALENDO HURU
Back To Top