Mtunzi:ENEA FAIDY
....
Shule ya sekondari Mabango ilikuwa na utulivu wa hali ya juu tangu
Doreen alipoondoka shuleni pale. Licha ya kwamba kulikuwa na upungufu wa
walimu lakini hali ilikuwa shwari kabisa. Wanafunzi waliendelea na
masomo yao kama kawaida huku wakimshukuru Mungu kwa kuwaondolea mbaya
wao aliyeisumbua shule ndani ya muda mfupi tu.
Majira
ya saa saba mchana katika shule ile alifika Mwanaume mmoja wa makamo
akiwa ameambatana na mwanamke mmoja mwembamba mrefu. Wanafunzi wa shule
waliokuwa karibu waliweza kugundua kuwa mwanamke yule bila shaka
alikuwa ni mama yake Dorice kwa jinsi walivyofanana. Nadia Joseph
aliyekuwa anapita eneo lile la ofisi aliwasalimia kwa heshima kisha
akasimama kidogo huku akitafakari jambo alilotaka kuzungumza.
"Samahani mama.. We ni ndugu yake Dorice.." Aliuliza Nadia huku akitabasamu.
"Ndio.. Ni mama yake mzazi.." Alijibu mama yule.
"Oh
mmefanana sana... Vipi lakini hajambo?" Aliuliza Nadia akiwa
anatabasamu lakini swali lile lilikuwa kama mwiba mkali moyoni mwa Mama
Dorice kwani ujio wake pale shuleni ilikuwa ni kumfuata Dorice na kupata
taarifa zake kwani ulipita muda mrefu sana bila mawasiliano yoyote.
"Kwani
Dorice hayupo hapa shule?" Aliuliza Mwanaume aliyeambatana na Mama
Dorice kwa mshangao. Na huyo alikuwa ni mjomba wa Dorice.
"Ah!
Unataka kuniambia hayupo nyumbani?" Alishangaa Nadia lakini ndani ya
muda mfupi alitokea madam Amina eneo lile hivyo Nadia aliamua kuondoka
ili kukwepa adhabu.
Madam
Amina aliwasogelea wageni wale na kuwasalimu. Kisha akawakaribisha
ofisini. Bila kuchelewa wageni wale waliambatana na Mwalimu Na kuingia
ofisini.
"Karibuni sana.. "
"Asante.. Sisi ni wazazi wa Dorice na tumekuja hapa kuuliza binti yetu anaendeleaje?"
"Dorice.. Alikuwa kidato cha nne?" Aliuliza mwalimu.
"Ndio!"
"Mmh!
Mbona aliacha shule na tuliwapigia simu mkasema amefika" alisema
Mwalimu Amina kwa mshangao. Kauli ile iliularua moyo wa mama Dorice na
kumfanya achanganyikiwe sana, maana hakuna simu aliyopigiwa wala
Kuambiwa chochote kuhusu mwanae.
"We mwalimu umechanganyikiwa? Mbona kama hujielewi eti?" Mama yule wa kinyaturu aliinuka kitini na kuanza kumfokea mwalimu.
Mwalim
Amina aliamua kujitetea kwani hali ya hewa ilianza kuchafuka ofisini
mle. "Tunamtaka mwanetu.. Mmemtorosha nyie? Au mmemuua?" Alizidi
kucharuka mama Dorice.
Mwalimu
Amina alikumbuka mbali, akakumbuka siku ambayo Dorice alipotea kisha
wakapewa taarifa za upotevu wa mwanafunzi huyo. Barua ya maelezo
iliandikwa kisha walimu wakapiga simu kwa wazazi wa Dorice. Lakini kwa
bahati mbaya sana simu ilipokelewa na jini Mansoor kwa namna ya ajabu
sana. Na jini huyo aliongea sauti ya Mama Dorice na kuwafanya walimu
wajiaminishe vizuri kuwa waliongea na mama Dorice lakini kumbe haikuwa
hivyo na hakuna aliyejua siri hiyo zaidi ya Mansoor pekee.
"Mama tena nilipiga simu Mimi.. Na ulikubali mwanao aache shule.." Alijitetea madam Amina lakini hakueleweka.
Wazazi
wa Dorice waliondoka kwa hasira sana shuleni pale huku wakiwa hawajui
binti yao alienda wapi. Roho iliwauma sana lakini hawakuwa na jinsi.
Waliondoka na gari yao waliokuwa wamekodi ikawafikisha kituo cha mabasi
Iringa mjini.
Walishuka
ili watafute sehemu ya kula chakula kwani hawakula chochote tangu
asubuhi kisha wakate tiketi, ghafla kwa mbali sana Mama Dorice alimwona
msichana kama Dorice. Alijifuta macho yake na kutazama vizuri akamtazama
vizuri binti yule.
"Kaka Dorice yule pale"
"Yuko wapi?" Kaka yake alishtuka sana.
"Pale
mbele kwenye watu wengi.. Tumfate haraka.." Alisema Mama Dorice akiwa
tayari ameanza kupiga hatua kuelekea kule alipo msichana yule.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )