MAHAKAMA Kuu ya Tanzania imetupilia mbali kesi iliyofunguliwa na Kampuni
ya Dubai Firm Rental Services &Solutions (RSS) dhidi ya Shirika la
Umeme Tanzania (Tanesco) na Kampuni ya Symbion Power Tanzania, ikizidai
fedha za malipo ya mtambo iliyowakodisha.
Hukumu ya kesi hiyo ambayo ilichukua vichwa vya habari kwenye vyombo vya habari nchini miezi kadhaa iliyopita, imetolewa na Mahakama Kuu wiki iliyopita. Aprili mwaka huu, Kampuni ya Rental Services and Solutions ya Dubai ilifungua kesi Mahakama Kuu dhidi ya Symbion Power na Tanesco.
RSS ilidai kampuni hizo zimeshindwa kulipa deni lake la Dola za Kimarekani milioni 28, ikiwa ni malipo ya ukodishaji mitambo na vifaa vyake vya umeme katika miradi ya umeme iliyokuwa inatekelezwa na Symbion katika maeneo mbalimbali nchini.
Hata hivyo Symbion ilipinga madai ya RSS kwa maelezo kuwa sheria za Tanzania zinawataka wafanyabiashara na watu wengine wanaofanya shughuli mbalimbali hapa nchini, kulipa kodi kutokana na shughuli zao.
Symbion ilidai kuwa RSS hawajalipa kodi, hivyo iliamua kukata kodi kwenye malipo yao na kuilipa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na iliahidi kuwalipa RSS fedha hizo iwapo wangetoa uthibitisho wa cheti kikionesha kuwa tayari wamelipa kodi kwa TRA.
Kutokana na malalamiko yao, Mahakama Kuu imetupilia mbali madai ya RSS hivyo kuwapa ushindi Symbion na Tanesco.
Akizungumza baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo, Makamu Mwenyekiti wa Kampuni ya Symbion anayehusika na Masuala ya Umma na Mawasiliano, Adi Raval alisema: “Maamuzi ya Mahakama Kuu yanadhihirisha na kuongeza uzito kwenye msimamo wa muda mrefu wa Symbion kwamba haya madai hayakuwa ya msingi. Hii ilikuwa ni kesi iliyolenga kuidhalilisha Kampuni ya Symbion na Tanesco."

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )