Msanii Diamond Platnumz
amefunguka na kuwataka wasanii ambao wanachipukia na wale ambao wapo
kwenye muziki wafikiri kufanya mambo zaidi yake na wasifikirie au kuwaza
kuwa kama Diamond Platnumz.
Diamond Platnumz alisema haya kwenye kipindi cha Planet bongo ya East
Africa Radio na kusema wasanii ambao watakuwa wakimuwaza yeye watakuwa
watumwa wake, lakini kama watafikiria kufanya vitu zaidi yake itasaidia
kwani itafanya kila mtu kuwa na njia yake na kuweza kufanikiwa zaidi
katika muziki wao pamoja na maisha kiujumla.
“Mimi nataka kuwaambia wasanii wafikirie kufanya vitu vikubwa zaidi wasifikirie kuwa kama Diamond Platnumz, maana kama watakuwa wanafikiria kuwa kama mimi watakuwa watumwa wa muziki wangu na maisha yangu, mfano unafikiri Wizkid angeamua wa ‘copy’ P Square ingekuwaje? Jibu angekuwa mtumwa wa P Square lakini kwa kuwa alitoka kivyake vyake ndiyo maana saizi Wizkid anafanya vizuri zaidi hata ya P Square ulimwenguni” alisema Diamond Platnumz.
eatv.tv

Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )