Wafuasi
wa Jean Ping wakpandishwa katika malori ya polisi, katika makao makuu ya
mgombea wa upinzani, tarehe 1 Septemba katika mji wa Libreville.
Vikosi
vya usalama nchini vimewaweka mbaroni watu zaidi ya elfu moja wakati wa
siku ya pili ya vurugu kufuatia uchaguzi wa rais. Watu watatu waliuawa
katika mji mkuu wa Gabon, Libreville.
Waandamanaji
waliokua wakiunga mkono kambi ya upinzani waliingia mitaani katika mji
mkuu wa Gabon muda mfupi baada ya kutangazwa ushindi wa Ali Bongo
Ondimba katika uchaguzi wa rais.
Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Marekani na Ufaransa wametoa wito kwa kuwepo na uwazi zaidi kuhusu matokeo ya uchaguzi.
Waziri wa
Mambo ya Ndani Pacome Moubelet Boubeya alisema Alhamisi wiki hii kwamba
watu 800 walikamatwa katika mji wa Libreville na wengine 400 katika
mikoa mingine.
Vikosi vya usalama vilitumwa baada ya jengo la Bunge kuchomwa moto na baada ya baadhi ya barabara kuu za mji kuzuiliwa.
Katika hotuba yake, Rais Bongo alisema: "Demokrasia hawezi kutumika kama bunge lake linashambuliwa."
Polisi
ililitumia mabomu ya machozi kutawanya umati wa watu na kuwakamata watu
waliokua wakitembea karibu na vifusi vya jengo la Bunge. RFI
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )