Wafuasi hao wameeleza kuwa wameamua kumzuia kwani Msajili wa Vyama vya Siasa ametaka shughuli zozote ndani ya CUF zisiendelee hadi hapo mgogoro wa uongozi utakapotatuliwa.
Itakumbukwa hivi karibuni CUF kilimteua Julius Sunday Mtatiro kuwa mwenyekiti wa muda baada ya mwenyekiti aliyekuwepo, Prof. Lipumba kijiuzulu Agosti 2015.
Julius Mtatiro leo amefanya mkutano na waandishi wa habari katika ofisi za Makao Makuu ya CUF, Buguruni, Dar es Salaam ili kuzungumzia kauli zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli akiwa visiwani Zanzibar.
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )