Mtunzi : Eddazaria g.Msulwa
Ilipoishia...
Roho
ya huruma ikaniingia na kujikuta nikianza kukimbia na kuwakumba watu
waliopo mbele yangu na kujikuta nikisimama gafla huku macho ni kiwa
nimeyatoa kiasi kwamba hasira ikazi kunipanda hii ni baada ya kumkuta ni
mama yangu ndio anaye pigwa na askari hawa wanao onekana hawana huruma
kabiasa wa watumwa walipo ndani ya hili pango.
Endelea....
Nikajirusha
juu ya mwili wa mama yangua na kumkumbatia kitendo kilicho zidisha
hasira ya askari hawa na wakaanza kunishambulia mimi kwa
kunipiga,sikaanza kusikia uzito mwengine ukija juu yangu na nikagundua
kuwa watumwa wengine wamepatawa na roho ya huruma na wao mwaneamua
kufanya kama nilivyo fanya mimi na kwa umoja wetu ikawalazimu askari
kusitisha zoezi lao la kutupiga.
Wakatuamuru
tuweze kurudi kwenye kazi za kuvunja miamba,nikamnyanyua mama taratibu
huku uso wake ukiwa umejawa na damu zilizo changanyikana na machozi
mengi.Nikamshika mama huku akiwa hatambui ni nani aliye mshika na kabla
sijamsemesha kitu cha ina yoyote askari mmoja anisukuma ili nimuechie
mama kisha akamshika mama mkono na kuanza kumburuza kitendo kilicho
zidi kunipandisha hasira ila kabla sijhamfwata nikastukia nikichapwa na
fimbo aina ya mkia wa taa iliyo jizungusha kwenye tumbo langu na
kunirudisha nyuma baada ya askari aliye nichapa kafanya hivyo bila ya
huruma.
Nikamshuhudia
mama akipotelea gizani kwenye pango pamoja na askari aliye mchukua na
sikuwa na lakufanya zaidi ya kuendelea kupokea kichapo cha kuchapwa
nikiamrishwa kwenda kufanya kazi upasuaji wa mame.Nikaokota moja ya
nyundo huku nikiwa na hasira na uchungu mwingi na kuaza kuvunja mwamba
amabao wenzangu wanaendelea kuuvunja.Kitu ambacho nimegundua ni kwamba
watu wengi waliomo humu ndani wamelishwa makaa ya mawe moto ambaya sio
rahisi kwa mtu kuweza kuzungumza chocheta zaidi ya kutoa miguno.
Hali
ya maisha ikazidi kuwa ngumu kwa upande wangu kadri ya siku zinavyo
zidi kwenda sikuweza kumuona mama yangu japo ninaendelea kufanya juhudi
ya kuchunguza ni wapi alipo mama na sikuwa ninafahamu kama yupo hai au
tayari amesha fariki,mwili wangu ukazidi kudhohofika kutokana na chakula
finyu tunacho pewa asubuhi na jiono,asabuhi tunakunywa kikombe kidogo
cha uji usio na kadha ya aina yoyote na usiku tunapewa viazi viwili
vilivyo chemshwa na huo ndio mlo wa siku moja na mbaya zaidi chakula ni
chakugombani usipo fanya hivyo unaweza kukaa siku mbili hadi tatu pasipo
kula.
Watu
wengi wanazidi kufa kutokana na njaa inayo andamana na kazi ngumu kwa
upande wangu kifua kianza kuniuma sana ikafikia hatua nikaanza kukohoa
na makohozi yangu yamechanganyikana na damu nyingi.
“hapana siwezi kufa humu ndani”
Nimawazo
ambayo yakawa yanajirudia rudia kichwani kwangu kadri siku zinavyo zidi
kwenda,mbaya zaidi sikuweza kujua upi ni usiku na upi ni mchana hii ni
kutokana na muda wote tuliopo ndani ya pango mataa makubwa yanawaka,kila
ninapo jitazama mwili wangu ninajikuta nikimwagikwa na machozi kwani
mbavu zangu unaweza kuzihesabu,mikono na miguu yangu imekondeana
sana.Nyele zangu zimekosa uhusiano mzuri kichwani vidonda vingi ambavyi
vingine vimefikia hadi hatua ya kutoka na funza vikaendelea kunitesa
mwili wangu.
“mungu wangu ninaomba unipe nguvu na juhudi katika hili”
Nikaanza
kufanya kazi ya kutafuta ni wapi ninaweza kupata njia ya kutokea na kwa
bahati nzuri katika uvunjaji wangu wa miamba nikaona sehemu yenye ufana
wenye kijisihimo kidogo,nikawatazama askari waliopo ndani humu na
hakuna aliye nifwatiliza nikapiga hatua za taratibu na kuchungulia
kwenye shimo na kuona mwanga kwa mbali na akili yangu ikatambua utakuwa
ni mwanga wa jua.
Kengele
ya kwenda kupata chakula cha jioni ikagongwa na nikatupa sururu niliyo
nayo chini na kuchomoja kwa kasi kuwania chakula ambacho nikikosa leo
itakuwa siku yangu ya pili kukosa chakula.Japo mwili wangu umedhohofika
nikajikaza katika kugombani viazi na kupata viazi vitatu,nikakaa kwenye
sehemu ambayo siku zote huwa ninapenda kukaa na kuanza kuvisakamia
viazi kwa fujo
Nikastukia
nikiguswa mguu na binti mdogo na akaniwekea mkono kwa ishara ya
kuniomba kiazi kimoja ambacho nimebaki nacho mkononi.Nikamtazama kwa
jinsi alivyo kondeana hadi sura yake imejaa vishimo shimo vilivyo kosa
nyma kwa kukondeana.Taratibu nikampa kijikiazi nilicho nacho na chote
akakiweka mdomoni na kuanza kukitafuna kwa haraka na inavyo onyesha ana
njaa kuliko mimi.Akanishukuru kwa kuikutanisha mikono yake kwa pamoja
huku akiinama na akanyanyuka taratibu na kuondoka.
Tukuruhusiwa
kwenda kulala kwenye mapango yetu ambayo milango yake ni ya chuma na
katika chumba kimoja cha pango tunalala watu si chini ya thelathini na
tangu niingie kwenye hili pango sikuwahi kuona hata siku moja watu
wakienda kuoga kwahi maji tunayo kunywa ni machafu sana na yapo kwenye
kijikisima kimoja kidogo.Harufu ya uchafu wa miili yetu siku zote
inanikusesha raha ya kulala na hususani loe kidogo ninajambo la
kuliwazia kichwani kwangu kutokana na ufana nilio uona ninaimani
utanisaidia katika kutoroka ndani ya hili pango.
Muda
wa kuamshwa ukawadia na tukatoka ndani ya vyomba vyetu na kuelekea
sehemu za utendaji wetu wa kazi na kitu cha kwanza kufika kwenye sehemu
yangu nikawa na kazi ya kuvujunya ufa nilio uona,ugumu wa mwamba huu
hakunifanya nife moyo zaidi ya nilicho kifanya ni kuendelea kuvunja hadi
ikafikia kipindi matumaini yakaaza kuja,filimbi ya dharura ikapangwa na
tukakusanyika kwenye eneo la moja na askari wakaanza kutupanga mistari
mitatu na tukasubiria nini tunacho taka kuambiwa.
Nikawaona
watu wanne walio valia vizuri na nikamgundua mmoja wao ambaye ni baba
yangu mkubwa mzee godwin akiwa ameongozana na watu wengine watatu ambao
sikuwajua.Mukuu wa askari wa eneo hili akawapokea kwa unyeyekevu mkubwa
na kuanza kuwapitisha kwa kwenye mistari mmoja baada ya mwengine kama
vile raisi anaye kagua gwaride la wanajeshi.
Sura
yangu nikaiinamisha chini ili asiweze kunijua kwa haraka na kabla ya
kunifikia mimi akahamia kwenye mstari wa nyuma yetu na kuendelea
kuwatazama watumwa wezangu tuliopo kwenye eneo hili,wakamaliza kazi hii
na wakapanda kwenye ofisi ya mkuu wa eneo hili huku wakizungumza na
kucheka kwa furaha.
Uchungu
na maumivu makali yakaendelea kuutesa moyo wangu ila sikuwa
jinsi,tukarudi kwenye sehemu zetu na kuendelea na kazi hata kengele ya
uji ilivyo gonga sikuwa na haja ya kwenda kugombania uji.Nikaendelea
kupasua mwamba huu na kugundua mawe haya nikiyagonganisha kwa pamoja
yanaweza yakazalisha moto kutokana na chechezake.Nikawaona askari wanao
tusimamia wakielekea walipo kwenda baba na wezake wakionekana kujawa na
furaha hapa ndipo nikaamini kuwa baba mkubwa ndio mmiliki wa hili eneo.
Kwa
bahati nzuri nikaona kamba moja ambayo hutumia katika kubutia mawe
makubwa,nikaichukua na kwenda moja kwa moja kwenye mapipa yenye mafuta
ya petrol ambayo yanatumika kuendeshea majenereta yanayo washa taa za
humu ndani,kwa haraka nikaichovya kamba kwenye pipa lenye mafuta na
kabla sijaondoka eneo lenye mapipa nikaona kidungu kidogo cha maji ya
lita moja na nusu.
Nikakiokota
na kuchota mafuta nusu na kurudi katika eneo lenye ufa,kwa uzuri ni
kwaba sehemu yenye ufa juu yake ndipo zilipo ofisi za wakuu wa hii
sehemu na haikuw ni raisi kwa wao kuniona kutokana nipo chini shana na
pameingia ndani.Wezangu tayari wamesha toka kunywa uji na wanaendelea na
kazi zao za upasuaji wa mawe na kelele za upasuaji wa mawe zikazidi
kunipa moyo wa kwamba sio rahisi kwa maaskari kuweza kusikia kitu cha
aina yoyote.
Nikaiingiza
kamba kwenye mdomo wa kidungu nilicho kiokota japo kamba ni nene kiasi
ila nikajitahidi kuigandamiza hivyo hivyo na ikaingia kiasi
kidogo.Nikakichomeka kidungu sehemu yenye ufa na kabla sija ondoka
kwenye eneo hili msichana aliye niomba kiazi jana usiku akanifwata na
kunigusa mkono na kwa ishara akaanza kunielekeza kitu ambacho haikuwa si
raisi kwa mimi kuielewa
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )